Follow us on
  • vimeo logo
Version internationale

Uchaguzi wa Mama mkuu: Jumapili, Julai 20.

21 Jul 2025

Leo ni siku ya Bwana na…kwa Mkutano, ni siku ya uchaguzi wa Mama Mkuu: siku ya ufufuko kwa namna mbili, anatuambia Padre Tournier!

Siku moja kabla, tulikuwa na siku ya mafungo, ya ukimya mkuu na kusikiliza Neno la Mungu, la kumkaribisha Roho Mtakatifu, ili kutambua chaguo la kila mmoja ili kutimiza utume wa Mama Mkuu wa mwaka 2025 hadi 2031. Pamoja na msalaba ukiwa umebebwa kudhihirisha kuelekea altareni.

Asubuhi ya leo, mara ya kwanza ikiwa siyo kawaida, Misa (pamoja na sala za Mwenyeheri Petro Vigne) inatangulia uchaguzi, huku mshumaa wa Pasaka ukibebwa kwa maandamano: ‘Mkutano mkuu ni adhimisho la Pasaka’. Hapa tunaelewa..

Wimbo wa Veni Creator(Njoo Roho Muumbaji)
Uliambatana na kuingia kwa washiriki wa Mkutano mkuu mwenye chumba cha Mkutano mahali ambapo uchaguzi hufanyika kwa mujibu wataratibu za Shirika. Mlio wa kengele na kuimba Te Deum vinaashiria kurudi kwa washiriki wa mkutano kwenye kanisani ili kutoa shukrani kwa kuchaguliwa kwa Sr Ana Ida Caso de Godoy kama Mama mkuu.

Kwa hiyo chakula ni cha cherehe…huku kukiwa na mashangilio mengi, matashi mema, na maua yanayotolewa kwa Mama mkuu mpya aliyechaguliwa. Vile vile tafrija iliyofuata, ilisikika kwa hisia, nyimbo za furaha, dansi ya urafiki na zawadi za shukrani kwa huduma ndefu na yenye matunda ya Sr Jailde Soares de Araujo, hasa safari ya kwenda hija Nchi Takatifu mnamo Oktoba 2025.

Alasiri iliendelea na ziara ya kwenda kuwatembelea masista wetu waliopo kwenye nyumba za kutunza wazee : Sr Marie Noëlle Rosa, Sr. Marie Cécile Feugier et Sr Marie Monique Bruyère huko L’Arnaud(Romans) na Sr Laurence Marie Meissimilly, Sr Marie Thérèse Dimulle na Sr Marie Elisabeth Audely huko Olivier (Valence). Mwishoni mwa chakula cha usiku pia tuliwapokea majirani zetu wapendwa, Baraza la Halmashauri la Masista wa Jésus Serviteur. Inavyopendeza, ilivyo vizuri masista kukaa pamoja! (Zab. 133)

Bwa

na atukuzwe na ahimidiwe kwa ajili ya siku hii iliyojaa Imani, matumaini na mapendo, kama ilivyotualika sala ya Kolekta ya liturujia ya siku.