Washiriki wa mkutano walipata fursa siku ya Jumapili iliyokuwa huru kwenda hija ya burudani huko Boucieu-le-Roi, kukiwa na hali nzuri sana ya hewa. Anga likiwa shwari na upepo wa kukaribisha viliruhusu baadhi ya masista wengine kwenda kujipatia maji kwenye chemchemi ya Padre Vigne, wengine kumtembelea Sr. Claude Marie Voignier huko Lamastre, na wote kufanya mazoezi ya utamaduni wa kukutana!… Kwenye mlo, na hata kwenye Misa iliyoadhimishwa katika kanisa la parokia, tulijumuika na Sr. Marie-José na Sr. Marie-Alice, pamoja na marafiki wa Shirika wanaoishi Boucieu na kandokando.
Masifu ya jioni yalihitimisha siku hii nzuri ya udugu na ya kupata nguvu mpya katika mahali papendwa pa msingi wetu. Tunacho cha kuendelea na mkutano wetu Valence! Lakini… usisahau kutuombea