Julai 13, 2025
Adhimisho la ufunguzi limewakutanisha pamoja wajumbe wa Mkutano katika Kanisa la Nyumba Mama (Valence) na marafiki wengi ili kumkabidhi Bwana kazi zote zijazo … na pia kushiriki furaha ya kusherehekea Jubilee ya dhahabu (miaka ya 60) ya Sr. Thérèse Marie Lafont.
Wakiingia kwa maandamano wakimfuata Sr. Jailde, Mkuu wa Shirika, na Sr Sheila na Sr Marie-Angelina, Washauri, masista ishirini na nane wajumbe wa Mkutano mkuu
walikamilisha kuweka logo ya mkutano mbele ya altare: Yesu ni Jua linaloongoza maisha ya Kanisa zima na Baba “hutupatia wakati ujao na tumaini,” kwa kulingana na maneno ya nabii Yeremia!
Tumaini (mada ya Mwaka wa Jubilee wa 2025) inaashiriwa na ndoano yenye nguvu kutoka kwa jahazi la huduma kwenye Rhône; matumaini yamekuwepo tangu siku za kwanza za kuanzishwa kwa Shirika na Petro Vigne na Masista saba waanzilishi. Na safari za wamisionari hazijakoma kamwe kwa muda wa miaka 310… Yajayo bado hayajapangwa bayana lakini yaliyopita yanatutajirisha na ya sasa yanatufundisha.
Kwa kuwa mtazamo wa upendo umewasha maisha yetu, wacha tuwashe siku zijazo kwa moto wa matumaini! Angalia vizuri!… Utawakuta Maria na Mwenyeheri Petro Vigne wakiwa tayari kutuongoza, usiku na mchana, wakiwa na nyota au mwanga wa mnara wa taa… Pia utaona kwamba hali ya sherehe haizuii macho yetu kukutana kwa kina… Na utaelewa nguvu ya baraka inapounganisha vitendo na maneno!
Asante kwa kuendelea kusindikiza Mkutano na sala yako.